PDF —
46 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura An-Nazi'at pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura An-Nazi'at pdf Kiswahili — Pakua Sura An-Nazi'at Tafsiri. Sura An-Nazi'at (Makka) 46 Aya.

← An-NabaSura An-Nazi'at Abasa →


46 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮢﮣﮤ
79:1 Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu,
ﮥﮦﮧ
79:2 Na kwa wanao toa kwa upole,
ﮨﮩﮪ
79:3 Na wanao ogelea,
ﮫﮬﮭ
79:4 Wakishindana mbio,
ﮮﮯﮰ
79:5 Wakidabiri mambo.
ﮱﯓﯔﯕ
79:6 Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka,
ﯖﯗﯘ
79:7 Kifuate cha kufuatia.
ﯙﯚﯛﯜ
79:8 Siku hiyo nyoyo zitapiga piga,
ﯝﯞﯟ
79:9 Macho yatainama chini.
ﯠﯡﯢﯣﯤﯥ
79:10 Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?
ﯦﯧﯨﯩﯪ
79:11 Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?
ﯫﯬﯭﯮﯯﯰ
79:12 Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara!
ﯱﯲﯳﯴﯵ
79:13 Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,
ﯶﯷﯸﯹ
79:14 Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
ﯺﯻﯼﯽﯾ
79:15 Je! Imekufikia hadithi ya Musa?
ﯿﰀﰁﰂﰃﰄﰅ
79:16 Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia:
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖ
79:17 Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.
ﭗﭘﭙﭚﭛﭜﭝ
79:18 Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?
ﭞﭟﭠﭡﭢ
79:19 Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.
ﭣﭤﭥﭦ
79:20 Basi alimwonyesha Ishara kubwa.
ﭧﭨﭩ
79:21 Lakini aliikadhibisha na akaasi.
ﭪﭫﭬﭭ
79:22 Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
ﭮﭯﭰ
79:23 Akakusanya watu akanadi.
ﭱﭲﭳﭴﭵ
79:24 Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.
ﭶﭷﭸﭹﭺﭻ
79:25 Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.
ﭼﭽﭾﭿﮀﮁﮂ
79:26 Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa.
ﮃﮄﮅﮆﮇﮈﮉﮊ
79:27 Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!
ﮋﮌﮍﮎ
79:28 Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.
ﮏﮐﮑﮒﮓ
79:29 Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake.
ﮔﮕﮖﮗﮘ
79:30 Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.
ﮙﮚﮛﮜﮝ
79:31 Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake,
ﮞﮟﮠ
79:32 Na milima akaisimamisha,
ﮡﮢﮣﮤ
79:33 Kwa nafuu yenu na mifugo yenu.
ﮥﮦﮧﮨﮩ
79:34 Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa,
ﮪﮫﮬﮭﮮﮯ
79:35 Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya,
ﮰﮱﯓﯔﯕ
79:36 Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,
ﯖﯗﯘﯙ
79:37 Basi ama yule aliye zidi ujeuri,
ﯚﯛﯜﯝ
79:38 Na akakhiari maisha ya dunia,
ﯞﯟﯠﯡﯢ
79:39 Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!
ﯣﯤﯥﯦﯧﯨﯩﯪﯫﯬ
79:40 Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,
ﯭﯮﯯﯰﯱ
79:41 Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!
ﯲﯳﯴﯵﯶﯷ
79:42 Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
ﯸﯹﯺﯻﯼ
79:43 Una nini wewe hata uitaje?
ﯽﯾﯿﰀ
79:44 Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
ﰁﰂﰃﰄﰅﰆ
79:45 Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu.
ﰇﰈﰉﰊﰋﰌﰍﰎﰏﰐ
79:46 Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema