42 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﭑﭒﭓ
80:1 Alikunja kipaji na akageuka,
ﭔﭕﭖﭗ
80:2 Kwa sababu alimjia kipofu!
ﭘﭙﭚﭛﭜ
80:3 Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
ﭝﭞﭟﭠﭡ
80:4 Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
ﭢﭣﭤﭥ
80:5 Ama ajionaye hana haja,
ﭦﭧﭨﭩ
80:6 Wewe ndio unamshughulikia?
ﭪﭫﭬﭭﭮ
80:7 Na si juu yako kama hakutakasika.
ﭯﭰﭱﭲﭳ
80:8 Ama anaye kujia kwa juhudi,
ﭴﭵﭶ
80:9 Naye anaogopa,
ﭷﭸﭹﭺ
80:10 Ndio wewe unampuuza?
ﭻﭼﭽﭾ
80:11 Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
ﭿﮀﮁﮂ
80:12 Basi anaye penda akumbuke.
ﮃﮄﮅﮆ
80:13 Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
ﮇﮈﮉ
80:14 Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
ﮊﮋﮌ
80:15 Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
ﮍﮎﮏ
80:16 Watukufu, wema.
ﮐﮑﮒﮓﮔ
80:17 Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
ﮕﮖﮗﮘﮙ
80:18 Kwa kitu gani amemuumba?
ﮚﮛﮜﮝﮞ
80:19 Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
ﮟﮠﮡﮢ
80:20 Kisha akamsahilishia njia.
ﮣﮤﮥﮦ
80:21 Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
ﮧﮨﮩﮪﮫ
80:22 Kisha apendapo atamfufua.
ﮬﮭﮮﮯﮰﮱ
80:23 La! Hajamaliza aliyo muamuru.
ﯓﯔﯕﯖﯗ
80:24 Hebu mtu na atazame chakula chake.
ﯘﯙﯚﯛﯜ
80:25 Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
ﯝﯞﯟﯠﯡ
80:26 Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
ﯢﯣﯤﯥ
80:27 Kisha tukaotesha humo nafaka,
ﯦﯧﯨ
80:28 Na zabibu, na mimea ya majani,
ﯩﯪﯫ
80:29 Na mizaituni, na mitende,
ﯬﯭﯮ
80:30 Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
ﯯﯰﯱ
80:31 Na matunda, na malisho ya wanyama;
ﯲﯳﯴﯵ
80:32 Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
ﯶﯷﯸﯹ
80:33 Basi utakapo kuja ukelele,
ﯺﯻﯼﯽﯾﯿ
80:34 Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
ﰀﰁﰂ
80:35 Na mamaye na babaye,
ﰃﰄﰅ
80:36 Na mkewe na wanawe -
ﰆﰇﰈﰉﰊﰋﰌ
80:37 Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
ﰍﰎﰏﰐ
80:38 Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
ﰑﰒﰓ
80:39 Zitacheka, zitachangamka;
ﰔﰕﰖﰗﰘ
80:40 Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
ﭑﭒﭓ
80:41 Giza totoro litazifunika,
ﭔﭕﭖﭗﭘ
80:42 Hao ndio makafiri watenda maovu.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema