PDF —
40 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura An-Naba pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura An-Naba pdf Kiswahili — Pakua Sura An-Naba Tafsiri. Sura An-Naba (Makka) 40 Aya.



40 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﭑﭒﭓ
78:1 WANAULIZANA nini?
ﭔﭕﭖﭗ
78:2 Ile khabari kuu,
ﭘﭙﭚﭛﭜ
78:3 Ambayo kwayo wanakhitalifiana.
ﭝﭞﭟ
78:4 La! Karibu watakuja jua.
ﭠﭡﭢﭣ
78:5 Tena la! Karibu watakuja jua.
ﭤﭥﭦﭧﭨ
78:6 Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko?
ﭩﭪﭫ
78:7 Na milima kama vigingi?
ﭬﭭﭮ
78:8 Na tukakuumbeni kwa jozi?
ﭯﭰﭱﭲ
78:9 Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
ﭳﭴﭵﭶ
78:10 Na tukaufanya usiku ni nguo?
ﭷﭸﭹﭺ
78:11 Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?
ﭻﭼﭽﭾﭿ
78:12 Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?
ﮀﮁﮂﮃ
78:13 Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto;
ﮄﮅﮆﮇﮈﮉ
78:14 Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni,
ﮊﮋﮌﮍﮎ
78:15 Ili tutoe kwayo nafaka na mimea,
ﮏﮐﮑ
78:16 Na mabustani yenye miti iliyo kamatana.
ﮒﮓﮔﮕﮖﮗ
78:17 Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake,
ﮘﮙﮚﮛﮜﮝﮞ
78:18 Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi,
ﮟﮠﮡﮢﮣ
78:19 Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango,
ﮤﮥﮦﮧﮨ
78:20 Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.
ﮩﮪﮫﮬﮭ
78:21 Hakika Jahannamu inangojea!
ﮮﮯﮰ
78:22 Kwa walio asi ndio makaazi yao,
ﮱﯓﯔﯕ
78:23 Wakae humo karne baada ya karne,
ﯖﯗﯘﯙﯚﯛﯜ
78:24 Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji,
ﯝﯞﯟﯠ
78:25 Ila maji yamoto sana na usaha,
ﯡﯢﯣ
78:26 Ndio jaza muwafaka.
ﯤﯥﯦﯧﯨﯩ
78:27 Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu.
ﯪﯫﯬﯭ
78:28 Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu.
ﯮﯯﯰﯱﯲ
78:29 Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika.
ﯳﯴﯵﯶﯷﯸ
78:30 Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!
ﭑﭒﭓﭔ
78:31 Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu,
ﭕﭖﭗ
78:32 Mabustani na mizabibu,
ﭘﭙﭚ
78:33 Na wake walio lingana nao,
ﭛﭜﭝ
78:34 Na bilauri zilizo jaa,
ﭞﭟﭠﭡﭢﭣﭤ
78:35 Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo -
ﭥﭦﭧﭨﭩﭪ
78:36 Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha.
ﭫﭬﭭﭮﭯﭰﭱﭲﭳﭴﭵﭶ
78:37 Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake!
ﭷﭸﭹﭺﭻﭼﭽﭾﭿﮀﮁﮂﮃﮄﮅﮆ
78:38 Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu.
ﮇﮈﮉﮊﮋﮌﮍﮎﮏﮐﮑ
78:39 Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi.
ﮒﮓﮔﮕﮖﮗﮘﮙﮚﮛﮜﮝﮞﮟﮠﮡ
78:40 Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo!

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema