PDF —
29 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura At-Takwir pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura At-Takwir pdf Kiswahili — Pakua Sura At-Takwir Tafsiri. Sura At-Takwir (Makka) 29 Aya.

← AbasaSura At-Takwir Al-Infitar →


29 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﭙﭚﭛﭜ
81:1 Jua litakapo kunjwa,
ﭝﭞﭟﭠ
81:2 Na nyota zikazimwa,
ﭡﭢﭣﭤ
81:3 Na milima ikaondolewa,
ﭥﭦﭧﭨ
81:4 Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,
ﭩﭪﭫﭬ
81:5 Na wanyama wa mwituni wakakusanywa,
ﭭﭮﭯﭰ
81:6 Na bahari zikawaka moto,
ﭱﭲﭳﭴ
81:7 Na nafsi zikaunganishwa,
ﭵﭶﭷﭸ
81:8 Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,
ﭹﭺﭻﭼ
81:9 Kwa kosa gani aliuliwa?
ﭽﭾﭿﮀ
81:10 Na madaftari yatakapo enezwa,
ﮁﮂﮃﮄ
81:11 Na mbingu itapo tanduliwa,
ﮅﮆﮇﮈ
81:12 Na Jahannamu itapo chochewa,
ﮉﮊﮋﮌ
81:13 Na Pepo ikasogezwa,
ﮍﮎﮏﮐﮑ
81:14 Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha.
ﮒﮓﮔﮕ
81:15 Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,
ﮖﮗﮘ
81:16 Zinazo kwenda, kisha zikajificha,
ﮙﮚﮛﮜ
81:17 Na kwa usiku unapo pungua,
ﮝﮞﮟﮠ
81:18 Na kwa asubuhi inapo pambazuka,
ﮡﮢﮣﮤﮥ
81:19 Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu,
ﮦﮧﮨﮩﮪﮫﮬ
81:20 Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi,
ﮭﮮﮯﮰ
81:21 Anaye t'iiwa, tena muaminifu.
ﮱﯓﯔﯕ
81:22 Na wala huyu mwenzenu hana wazimu.
ﯖﯗﯘﯙﯚ
81:23 Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
ﯛﯜﯝﯞﯟﯠ
81:24 Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu.
ﯡﯢﯣﯤﯥﯦ
81:25 Wala hii si kauli ya Shetani maluuni.
ﯧﯨﯩ
81:26 Basi mnakwenda wapi?
ﯪﯫﯬﯭﯮﯯ
81:27 Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
ﯰﯱﯲﯳﯴﯵ
81:28 Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.
ﯶﯷﯸﯹﯺﯻﯼﯽﯾ
81:29 Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema