PDF —
17 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura At-Tariq pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura At-Tariq pdf Kiswahili — Pakua Sura At-Tariq Tafsiri. Sura At-Tariq (Makka) 17 Aya.



17 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﭑﭒﭓ
86:1 Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
ﭔﭕﭖﭗﭘ
86:2 Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
ﭙﭚﭛ
86:3 Ni Nyota yenye mwanga mkali.
ﭜﭝﭞﭟﭠﭡﭢ
86:4 Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.
ﭣﭤﭥﭦﭧ
86:5 Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
ﭨﭩﭪﭫﭬ
86:6 Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
ﭭﭮﭯﭰﭱﭲ
86:7 Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
ﭳﭴﭵﭶﭷ
86:8 Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
ﭸﭹﭺﭻ
86:9 Siku zitakapo dhihirishwa siri.
ﭼﭽﭾﭿﮀﮁﮂ
86:10 Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
ﮃﮄﮅﮆ
86:11 Naapa kwa mbingu yenye marejeo!
ﮇﮈﮉﮊ
86:12 Na kwa ardhi inayo pasuka!
ﮋﮌﮍﮎ
86:13 Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
ﮏﮐﮑﮒ
86:14 Wala si mzaha.
ﮓﮔﮕﮖ
86:15 Hakika wao wanapanga mpango.
ﮗﮘﮙ
86:16 Na Mimi napanga mpango.
ﮚﮛﮜﮝﮞ
86:17 Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema