PDF —
36 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-Mutaffifin pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-Mutaffifin pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Mutaffifin Tafsiri. Sura Al-Mutaffifin (Makka) 36 Aya.

← Al-InfitarSura Al-Mutaffifin Al-Inshiqaq →


36 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﯖﯗﯘ
83:1 Ole wao hao wapunjao!
ﯙﯚﯛﯜﯝﯞﯟ
83:2 Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
ﯠﯡﯢﯣﯤﯥ
83:3 Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.
ﯦﯧﯨﯩﯪﯫ
83:4 Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa
ﭑﭒﭓ
83:5 Katika Siku iliyo kuu,
ﭔﭕﭖﭗﭘﭙ
83:6 Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?
ﭚﭛﭜﭝﭞﭟﭠ
83:7 Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.
ﭡﭢﭣﭤﭥ
83:8 Unajua nini Sijjin?
ﭦﭧﭨ
83:9 Kitabu kilicho andikwa.
ﭩﭪﭫﭬ
83:10 Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!
ﭭﭮﭯﭰﭱ
83:11 Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
ﭲﭳﭴﭵﭶﭷﭸﭹ
83:12 Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.
ﭺﭻﭼﭽﭾﭿﮀﮁ
83:13 Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!
ﮂﮃﮄﮅﮆﮇﮈﮉﮊﮋﮌ
83:14 Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma.
ﮍﮎﮏﮐﮑﮒﮓ
83:15 Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.
ﮔﮕﮖﮗﮘ
83:16 Kisha wataingia Motoni!
ﮙﮚﮛﮜﮝﮞﮟﮠ
83:17 Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha.
ﮡﮢﮣﮤﮥﮦﮧ
83:18 Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin.
ﮨﮩﮪﮫﮬ
83:19 Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin?
ﮭﮮﮯ
83:20 Kitabu kilicho andikwa.
ﮰﮱﯓ
83:21 Wanakishuhudia walio karibishwa.
ﯔﯕﯖﯗﯘ
83:22 Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
ﯙﯚﯛﯜ
83:23 Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
ﯝﯞﯟﯠﯡﯢ
83:24 Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
ﯣﯤﯥﯦﯧ
83:25 Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,
ﯨﯩﯪﯫﯬﯭﯮﯯ
83:26 Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana.
ﯰﯱﯲﯳ
83:27 Na mchanganyiko wake ni Tasniim,
ﯴﯵﯶﯷﯸ
83:28 Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa.
ﯹﯺﯻﯼﯽﯾﯿﰀﰁ
83:29 Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini.
ﰂﰃﰄﰅﰆ
83:30 Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana.
ﰇﰈﰉﰊﰋﰌﰍ
83:31 Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
ﰎﰏﰐﰑﰒﰓﰔ
83:32 Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea.
ﰕﰖﰗﰘﰙ
83:33 Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖﭗ
83:34 Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,
ﭘﭙﭚﭛ
83:35 Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.
ﭜﭝﭞﭟﭠﭡﭢ
83:36 Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema