PDF —
50 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-Mursalat pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-Mursalat pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Mursalat Tafsiri. Sura Al-Mursalat (Makka) 50 Aya.

← Al-InsanSura Al-Mursalat An-Naba →


50 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮑﮒﮓ
77:1 Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
ﮔﮕﮖ
77:2 Na zinazo vuma kwa kasi!
ﮗﮘﮙ
77:3 Na zikaeneza maeneo yote!
ﮚﮛﮜ
77:4 Na zinazo farikisha zikatawanya!
ﮝﮞﮟ
77:5 Na zinazo peleka mawaidha!
ﮠﮡﮢﮣ
77:6 Kwa kuudhuru au kuonya,
ﮤﮥﮦﮧ
77:7 Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
ﮨﮩﮪﮫ
77:8 Wakati nyota zitakapo futwa,
ﮬﮭﮮﮯ
77:9 Na mbingu zitakapo pasuliwa,
ﮰﮱﯓﯔ
77:10 Na milima itakapo peperushwa,
ﯕﯖﯗﯘ
77:11 Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,
ﯙﯚﯛﯜ
77:12 Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
ﯝﯞﯟ
77:13 Kwa siku ya kupambanua!
ﯠﯡﯢﯣﯤﯥ
77:14 Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
ﯦﯧﯨﯩ
77:15 Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
ﯪﯫﯬﯭ
77:16 Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
ﯮﯯﯰﯱ
77:17 Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?
ﯲﯳﯴﯵ
77:18 Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
ﯶﯷﯸﯹ
77:19 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖ
77:20 Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
ﭗﭘﭙﭚﭛ
77:21 Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
ﭜﭝﭞﭟ
77:22 Mpaka muda maalumu?
ﭠﭡﭢﭣ
77:23 Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
ﭤﭥﭦﭧ
77:24 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
ﭨﭩﭪﭫﭬ
77:25 Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
ﭭﭮﭯ
77:26 Walio hai na maiti?
ﭰﭱﭲﭳﭴﭵﭶﭷ
77:27 Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
ﭸﭹﭺﭻ
77:28 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
ﭼﭽﭾﭿﮀﮁﮂ
77:29 Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
ﮃﮄﮅﮆﮇﮈﮉ
77:30 Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
ﮊﮋﮌﮍﮎﮏﮐ
77:31 Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
ﮑﮒﮓﮔﮕ
77:32 Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
ﮖﮗﮘﮙ
77:33 Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
ﮚﮛﮜﮝ
77:34 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
ﮞﮟﮠﮡﮢ
77:35 Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
ﮣﮤﮥﮦﮧ
77:36 Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
ﮨﮩﮪﮫ
77:37 Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
ﮬﮭﮮﮯﮰﮱﯓ
77:38 Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
ﯔﯕﯖﯗﯘﯙ
77:39 Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
ﯚﯛﯜﯝ
77:40 Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
ﯞﯟﯠﯡﯢﯣ
77:41 Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
ﯤﯥﯦﯧ
77:42 Na matunda wanayo yapenda,
ﯨﯩﯪﯫﯬﯭﯮ
77:43 Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
ﯯﯰﯱﯲﯳ
77:44 Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.
ﯴﯵﯶﯷ
77:45 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
ﯸﯹﯺﯻﯼﯽ
77:46 Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
ﯾﯿﰀﰁ
77:47 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
ﰂﰃﰄﰅﰆﰇﰈ
77:48 Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
ﰉﰊﰋﰌ
77:49 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
ﰍﰎﰏﰐﰑ
77:50 Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema