PDF —
30 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-Fajr pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-Fajr pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Fajr Tafsiri. Sura Al-Fajr (Makka) 30 Aya.



30 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﭤﭥ
89:1 Naapa kwa alfajiri,
ﭦﭧﭨ
89:2 Na kwa masiku kumi,
ﭩﭪﭫ
89:3 Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja,
ﭬﭭﭮﭯ
89:4 Na kwa usiku unapo pita,
ﭰﭱﭲﭳﭴﭵﭶ
89:5 Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?
ﭷﭸﭹﭺﭻﭼﭽ
89:6 Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di?
ﭾﭿﮀﮁ
89:7 Wa Iram, wenye majumba marefu?
ﮂﮃﮄﮅﮆﮇﮈ
89:8 Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?
ﮉﮊﮋﮌﮍﮎ
89:9 Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni?
ﮏﮐﮑﮒ
89:10 Na Firauni mwenye vigingi?
ﮓﮔﮕﮖﮗ
89:11 Ambao walifanya jeuri katika nchi?
ﮘﮙﮚﮛ
89:12 Wakakithirisha humo ufisadi?
ﮜﮝﮞﮟﮠﮡ
89:13 Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.
ﮢﮣﮤﮥ
89:14 Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.
ﮦﮧﮨﮩﮪﮫﮬﮭﮮﮯﮰﮱ
89:15 Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!
ﯓﯔﯕﯖﯗﯘﯙﯚﯛﯜﯝ
89:16 Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!
ﯞﯟﯠﯡﯢﯣﯤ
89:17 Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima,
ﯥﯦﯧﯨﯩﯪ
89:18 Wala hamhimizani kulisha masikini;
ﯫﯬﯭﯮﯯ
89:19 Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa,
ﯰﯱﯲﯳﯴ
89:20 Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.
ﯵﯶﯷﯸﯹﯺﯻﯼ
89:21 Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande,
ﯽﯾﯿﰀﰁﰂ
89:22 Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu,
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖﭗﭘﭙﭚﭛ
89:23 Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?
ﭜﭝﭞﭟﭠ
89:24 Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu!
ﭡﭢﭣﭤﭥﭦ
89:25 Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.
ﭧﭨﭩﭪﭫ
89:26 Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.
ﭬﭭﭮﭯ
89:27 Ewe nafsi iliyo tua!
ﭰﭱﭲﭳﭴﭵ
89:28 Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha.
ﭶﭷﭸﭹ
89:29 Basi ingia miongoni mwa waja wangu,
ﭺﭻﭼ
89:30 Na ingia katika Pepo yangu.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema