Sura Al-Ghashiya kwa Kiarabu na Kiswahili

Soma Sura Al-Ghashiya na tafsiri kamili ya Kiswahili, maandishi na usomaji wa sauti. Tafsiri aya kwa aya. (26 Aya — مكية). Al-Ghashiya Sikiliza, Al-Ghashiya Tafsiri, Al-Ghashiya mp3, Al-Ghashiya pdf.

Soma na Sikiliza Sura Al-Ghashiya

🎧 Aya
M Mishary Rashid Alafasy
M Mahmoud Khalil Al-Husary
A Abdurrahman As-Sudais
M Mohamed Siddiq Al-Minshawi
A Abdul Basit Abdul Samad
A Ali Al-Hudhaify
A Ahmed ibn Ali al-Ajamy
A Abu Bakr Ash-Shaatree
M Muhammad Ayyoub
A Abdullah Basfar
A Abdullah Al-Juhani
M Maher Al Muaiqly
x1
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ ۝١
📖 Tafsiri Aya 1
Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ ۝٢
📖 Tafsiri Aya 2
Siku hiyo nyuso zitainama,
عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ ۝٣
📖 Tafsiri Aya 3
Zikifanya kazi, nazo taabani.
تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً ۝٤
📖 Tafsiri Aya 4
Ziingie katika Moto unao waka -
تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ ۝٥
📖 Tafsiri Aya 5
Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ ۝٦
📖 Tafsiri Aya 6
Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ ۝٧
📖 Tafsiri Aya 7
Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ ۝٨
📖 Tafsiri Aya 8
Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ ۝٩
📖 Tafsiri Aya 9
Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ۝١٠
📖 Tafsiri Aya 10
Katika Bustani ya juu.
لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً ۝١١
📖 Tafsiri Aya 11
Hawatasikia humo upuuzi.
فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ ۝١٢
📖 Tafsiri Aya 12
Humo imo chemchem inayo miminika.
فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ ۝١٣
📖 Tafsiri Aya 13
Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ ۝١٤
📖 Tafsiri Aya 14
Na bilauri zilizo pangwa,
وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ ۝١٥
📖 Tafsiri Aya 15
Na matakia safu safu,
وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ ۝١٦
📖 Tafsiri Aya 16
Na mazulia yaliyo tandikwa.
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ۝١٧
📖 Tafsiri Aya 17
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ ۝١٨
📖 Tafsiri Aya 18
Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ ۝١٩
📖 Tafsiri Aya 19
Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ ۝٢٠
📖 Tafsiri Aya 20
Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ ۝٢١
📖 Tafsiri Aya 21
Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ ۝٢٢
📖 Tafsiri Aya 22
Wewe si mwenye kuwatawalia.
إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ ۝٢٣
📖 Tafsiri Aya 23
Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,
فَيُعَذِّبُهُ اللَّهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ ۝٢٤
📖 Tafsiri Aya 24
Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ ۝٢٥
📖 Tafsiri Aya 25
Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم ۝٢٦
📖 Tafsiri Aya 26
Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!
← 87 Al-Ghashiya (88/114) 89 →
Soma Sura Al-Ghashiya kwa Kiswahili – Tafsiri na Sauti

88الغاشية Al-Ghashiyah 📚 26 Aya مكية



Kurani Tukufu


Tuesday, August 18, 2026

Usitusahau katika dua zako njema