PDF —
20 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-Balad pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-Balad pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Balad Tafsiri. Sura Al-Balad (Makka) 20 Aya.



20 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﭽﭾﭿﮀﮁ
90:1 Naapa kwa Mji huu!
ﮂﮃﮄﮅﮆ
90:2 Nawe unaukaa Mji huu.
ﮇﮈﮉﮊ
90:3 Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa.
ﮋﮌﮍﮎﮏﮐ
90:4 Hakika tumemuumba mtu katika taabu.
ﮑﮒﮓﮔﮕﮖﮗ
90:5 Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?
ﮘﮙﮚﮛﮜ
90:6 Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
ﮝﮞﮟﮠﮡﮢ
90:7 Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
ﮣﮤﮥﮦﮧ
90:8 Kwani hatukumpa macho mawili?
ﮨﮩﮪ
90:9 Na ulimi, na midomo miwili?
ﮫﮬﮭ
90:10 Na tukambainishia zote njia mbili?
ﮮﮯﮰﮱ
90:11 Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
ﯓﯔﯕﯖﯗ
90:12 Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?
ﯘﯙﯚ
90:13 Kumkomboa mtumwa;
ﯛﯜﯝﯞﯟﯠﯡ
90:14 Au kumlisha siku ya njaa
ﯢﯣﯤﯥ
90:15 Yatima aliye jamaa,
ﯦﯧﯨﯩﯪ
90:16 Au masikini aliye vumbini.
ﯫﯬﯭﯮﯯﯰﯱﯲﯳﯴ
90:17 Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
ﯵﯶﯷﯸ
90:18 Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖﭗ
90:19 Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.
ﭘﭙﭚﭛ
90:20 Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema