PDF —
15 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Ash-Shams pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Ash-Shams pdf Kiswahili — Pakua Sura Ash-Shams Tafsiri. Sura Ash-Shams (Makka) 15 Aya.

← Al-BaladSura Ash-Shams Al-Layl →


15 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﭜﭝﭞ
91:1 Naapa kwa jua na mwangaza wake!
ﭟﭠﭡﭢ
91:2 Na kwa mwezi unapo lifuatia!
ﭣﭤﭥﭦ
91:3 Na kwa mchana unapo lidhihirisha!
ﭧﭨﭩﭪ
91:4 Na kwa usiku unapo lifunika!
ﭫﭬﭭﭮ
91:5 Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!
ﭯﭰﭱﭲ
91:6 Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!
ﭳﭴﭵﭶ
91:7 Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!
ﭷﭸﭹﭺ
91:8 Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,
ﭻﭼﭽﭾﭿ
91:9 Hakika amefanikiwa aliye itakasa,
ﮀﮁﮂﮃﮄ
91:10 Na hakika amekhasiri aliye iviza.
ﮅﮆﮇﮈ
91:11 Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,
ﮉﮊﮋﮌ
91:12 Alipo simama mwovu wao mkubwa,
ﮍﮎﮏﮐﮑﮒﮓﮔ
91:13 Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.
ﮕﮖﮗﮘﮙﮚﮛﮜ
91:14 Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.
ﮝﮞﮟﮠ
91:15 Wala Yeye haogopi matokeo yake.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema