PDF —
60 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Adh-Dhariyat pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Adh-Dhariyat pdf Kiswahili — Pakua Sura Adh-Dhariyat Tafsiri. Sura Adh-Dhariyat (Makka) 60 Aya.

← QafSura Adh-Dhariyat At-Tur →


60 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﯤﯥﯦ
51:1 Naapa kwa pepo zinazo tawanya,
ﯧﯨﯩ
51:2 Na zinazo beba mizigo,
ﯪﯫﯬ
51:3 Na zinazo kwenda kwa wepesi.
ﯭﯮﯯ
51:4 Na zinazo gawanya kwa amri,
ﯰﯱﯲﯳ
51:5 Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli,
ﯴﯵﯶﯷ
51:6 Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.
ﭑﭒﭓﭔ
51:7 Naapa kwa mbingu zenye njia,
ﭕﭖﭗﭘﭙ
51:8 Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana.
ﭚﭛﭜﭝﭞ
51:9 Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.
ﭟﭠﭡ
51:10 Wazushi wameangamizwa.
ﭢﭣﭤﭥﭦﭧ
51:11 Ambao wameghafilika katika ujinga.
ﭨﭩﭪﭫﭬ
51:12 Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?
ﭭﭮﭯﭰﭱﭲ
51:13 Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni.
ﭳﭴﭵﭶﭷﭸﭹﭺ
51:14 Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza.
ﭻﭼﭽﭾﭿﮀ
51:15 Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
ﮁﮂﮃﮄﮅﮆﮇﮈﮉﮊﮋ
51:16 Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.
ﮌﮍﮎﮏﮐﮑﮒ
51:17 Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.
ﮓﮔﮕﮖ
51:18 Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.
ﮗﮘﮙﮚﮛﮜ
51:19 Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba.
ﮝﮞﮟﮠﮡ
51:20 Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
ﮢﮣﮤﮥﮦﮧ
51:21 Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?
ﮨﮩﮪﮫﮬﮭ
51:22 Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa.
ﮮﮯﮰﮱﯓﯔﯕﯖﯗﯘ
51:23 Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.
ﯙﯚﯛﯜﯝﯞﯟ
51:24 Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa?
ﯠﯡﯢﯣﯤﯥﯦﯧﯨﯩﯪ
51:25 Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.
ﯫﯬﯭﯮﯯﯰﯱ
51:26 Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.
ﯲﯳﯴﯵﯶﯷ
51:27 Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?
ﯸﯹﯺﯻﯼﯽﯾﯿﰀﰁﰂﰃ
51:28 Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu.
ﰄﰅﰆﰇﰈﰉﰊﰋﰌﰍ
51:29 Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa!
ﰎﰏﰐﰑﰒﰓﰔﰕﰖﰗ
51:30 Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua.
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖﭗ
51:31 AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa?
ﭘﭙﭚﭛﭜﭝﭞ
51:32 Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu,
ﭟﭠﭡﭢﭣﭤ
51:33 Tuwatupie mawe ya udongo,
ﭥﭦﭧﭨﭩ
51:34 Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka.
ﭪﭫﭬﭭﭮﭯﭰ
51:35 Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini.
ﭱﭲﭳﭴﭵﭶﭷﭸ
51:36 Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!
ﭹﭺﭻﭼﭽﭾﭿﮀ
51:37 Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu.
ﮁﮂﮃﮄﮅﮆﮇﮈﮉ
51:38 Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi.
ﮊﮋﮌﮍﮎﮏﮐ
51:39 Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!
ﮑﮒﮓﮔﮕﮖﮗﮘ
51:40 Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.
ﮙﮚﮛﮜﮝﮞﮟﮠ
51:41 Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi.
ﮡﮢﮣﮤﮥﮦﮧﮨﮩﮪ
51:42 Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka.
ﮫﮬﮭﮮﮯﮰﮱﯓﯔ
51:43 Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.
ﯕﯖﯗﯘﯙﯚﯛﯜﯝ
51:44 Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona.
ﯞﯟﯠﯡﯢﯣﯤﯥ
51:45 Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.
ﯦﯧﯨﯩﯪﯫﯬﯭﯮﯯ
51:46 Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.
ﯰﯱﯲﯳﯴﯵ
51:47 Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua.
ﯶﯷﯸﯹﯺ
51:48 Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!
ﯻﯼﯽﯾﯿﰀﰁﰂ
51:49 Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.
ﰃﰄﰅﰆﰇﰈﰉﰊﰋﰌ
51:50 Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
ﰍﰎﰏﰐﰑﰒﰓﰔﰕﰖﰗﰘﰙ
51:51 Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖﭗﭘﭙﭚﭛﭜﭝﭞ
51:52 Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu.
ﭟﭠﭡﭢﭣﭤﭥﭦ
51:53 Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.
ﭧﭨﭩﭪﭫﭬ
51:54 Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi.
ﭭﭮﭯﭰﭱﭲ
51:55 Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
ﭳﭴﭵﭶﭷﭸﭹ
51:56 Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.
ﭺﭻﭼﭽﭾﭿﮀﮁﮂﮃ
51:57 Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.
ﮄﮅﮆﮇﮈﮉﮊﮋ
51:58 Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.
ﮌﮍﮎﮏﮐﮑﮒﮓﮔﮕ
51:59 Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize.
ﮖﮗﮘﮙﮚﮛﮜﮝ
51:60 Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema