PDF —
19 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-'Alaq pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-'Alaq pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-'Alaq Tafsiri. Sura Al-'Alaq (Makka) 19 Aya.

← At-TinSura Al-'Alaq Al-Qadr →


19 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮕﮖﮗﮘﮙﮚ
96:1 Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
ﮛﮜﮝﮞﮟ
96:2 Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
ﮠﮡﮢﮣ
96:3 Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
ﮤﮥﮦﮧ
96:4 Ambaye amefundisha kwa kalamu.
ﮨﮩﮪﮫﮬﮭ
96:5 Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
ﮮﮯﮰﮱﯓ
96:6 Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri
ﯔﯕﯖﯗ
96:7 Akijiona katajirika.
ﯘﯙﯚﯛﯜ
96:8 Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
ﯝﯞﯟﯠ
96:9 Umemwona yule anaye mkataza
ﯡﯢﯣﯤ
96:10 Mja anapo sali?
ﯥﯦﯧﯨﯩﯪ
96:11 Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
ﯫﯬﯭﯮ
96:12 Au anaamrisha uchamngu?
ﭑﭒﭓﭔﭕ
96:13 Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
ﭖﭗﭘﭙﭚﭛ
96:14 Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
ﭜﭝﭞﭟﭠﭡﭢ
96:15 Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
ﭣﭤﭥﭦ
96:16 Shungi la uwongo, lenye makosa!
ﭧﭨﭩ
96:17 Basi na awaite wenzake!
ﭪﭫﭬ
96:18 Nasi tutawaita Mazabania!
ﭭﭮﭯﭰﭱﭲﭳ
96:19 Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee!

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema